PONGEZI: Charles Boniface Mkwasa na Betty Mkwasa kwa kutimiza miaka 25 ya ndoa yenu

PONGEZI: Charles Boniface Mkwasa na Betty Mkwasa kwa kutimiza miaka 25 ya ndoa yenu
January 19 00:29 2014 Print This Article

mkwasaKwa niaba ya wadau wote wa Jukwaa Huru Media Inc. napenda kuchukua fursa hii kuwatakia kila lakheri Bw. Charles Boniface Mkwasa, ambaye ni kocha maarufu nchini, pamoja na bi. Betty Mkwasa, mwanahabari mkongwe na hivi sasa mheshimiwa Mkuu wa wilaya, kwa wawili hao kuadhimisha miaka 25 ya ndoa yao.

Inatia moyo sana kuwa, wale ambao ni viongozi wetu kama wawili hawa, wanaonyesha mfano mzuri wa namna gani maisha ya ndoa yanatakiwa kujaa kuvumiliana na kuelewana hadi muweze kudumu kwa muda mrefu, na ninaamini kuwa mtaendelea kuwa hazina muhimu kwetu wengine kuchota busara, hekima na miongozo toka kwenu ili nasi tuweze kudumu na tulio nao.

Hongera sana na Mungu awajaalie maisha marefu ya ndoa, yenye uvumilivu, maelewano zaidi na inshaalah, tuje sherehekea miaka mingine 25 ijayo mkiwa na nyuso za furaha kama leo

VN:F [1.9.22_1171]
Rating: 0.0/10 (0 votes cast)
VN:F [1.9.22_1171]
Rating: 0 (from 0 votes)
  Categories:
write a comment

0 Comments

No Comments Yet!

You can be the one to start a conversation.

Add a Comment

Your data will be safe! Your e-mail address will not be published. Also other data will not be shared with third person.
All fields are required.